Facebook

Friday, December 1, 2023

HOSPITAL YA KUMBUKUMBU YA CHRLES KULWA YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 






Hospital ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa Iliyopo katika Kata ya Uyovu Wilaya ya         Bukombe Mkoani  Geita Imeendesha Zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyo yakuambukiza kwa watu wa jinsia zote wenye umri wa kuanzia miaka hamsini na kuendele akizIndua kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Said Nkumba alisema kuwa  Upimaji  huo umelenga kupima  magonjwa matatu ambayo ni  Kisukari, Tezi dume pamoja na Shinikizo ladamu (presha).
Akizungumza na wazee waliojitokeza katika zoezi hilo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa walichokifanya Hospital ya Kumbuklumbu ya Charles Kulwa ni kitendo cha pekee na cha kuigwa kwa kwani magonjwa hayo yamekuwa ni mwiba mkali kwa wazee hivyo wazee hao watapimwa bure na kisha kupatiwa huduma bure
 “Niwapongeze kwa huduma hii mnaoitoa  kwa jamii yetu kwani mnafanya zoezi kubwa la huduma ya upimaji kwa wananchi  kuweza kupima  magonjwa yasiyoambukiza wananchi wetu wa kata hii ya uyovu” Alisema Mkuu wa Wilaya hiyo Nkumba

 

kushoto ni mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe,Said Nkumba akifanyiwa kipimo cha presha na nesi mmoja kati ya wafanyakazi wa Hospital ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa

 Kwa upande wake Said Lugeyo mmoja wa Wazee waliopatiwa huduma hiyo alisema kuwa anaipongeza hospital ya kumbukumbu ya Charles Kulwa chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dr. Baraka Kulwa kwa jinsi  ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa jamii yetu ya Uyovu.

Aidha amemtaka aendelee na moyo huo huo wa kuwathamini Wazee ambayo hawana kipato cha kuweza kujitibia  lakini ni wagonjwa.

“Anayoyafanya kijana huyu Dr. Baraka yalikuwa yakifanywa miaka ya nyuma sana na marehemu wazazi wake hivyo jambo hilo ni ishara kubwa kijana huyu amelelewa katika misingi ya maadili mema yenye kuwathamini wazee” Alisema

Mmoja kati ya wazee waliojitokeza kupima akifanyiwa vipimo vya radiolojia



Naye Mkurugenzi wa Hospital ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa  Dr. Baraka Kulwa  ameeleza kuwa Lengo la zoezi la Upimaji huo kutoa shukuru kwa Wazazi wake wote wa kata hiyo ambao waliishi vizuri na waanzilishi wa hospital hiyo .

Aidha Dr. Baraka  amewataka wananchi wenye Umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea kujitokeza kwa wingi kupima magonjwa hayo kwani yamekuwa ni tatizo kwa jamii kwa watua wenye umri mkubwa,

pia alisema kuwa zoezi hili litakuwa ni endelevu kwa kuwapima wazee na tunakusudia kufanya mara mbili kwa mwaka yaani mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka kwa kusudi la kuwasaidia wazee wetu kuweza kutambua Afya zao.

Kulia ni Mkurugenzi wa Hospital ya kumbukumbu ya Charles Kulwa Akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe, Saidi Nkumba kabla ya uzinduzi ya magonjwa yasiyoambukiza



                        

Mamia ya wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo la upimaji wakisubiri huduma




0 Comments:

Post a Comment