Ikiwa ni miaka 52 sasa toka kuanzishwa shirika
la bima hapa nchini, bado watu wengi nchini Tanzania hawana uelewa juu ya
masuala ya bima ya afya. Mengi yametajwa kuwa chanzo cha wengi kushindwa
kujisajili ama kukata bima ya afya nchini. Miongoni mwa sababu zinazotajwa sana
ni ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu bima , umaskini uliotopea wa kutokujua
umuhimu wa bima ya afya katika dunia ya leo.
Ukweli haupingiki kuwa kukata bima ya afya kunahitaji kuwa na pesa na ni gharama kiasi
lakini kwa kuangalia faida zake kwa mahitaji ya mbeleni ni wazi ni jambo
mtambuka kulifanya.
Bima ya afya
ni mkataba wenye taswira mbili kwa upande mmoja unaofanana sana na aina
nyingine za mikataba kama ilivyo kwa mkataba wa watu wawili kuuziana baiskeli
kuingia ubia ili kushirikiana katika kuendesha biashara na kadhalika.
Malengo makuu ya uwepo wa bima ya afya ni kumnusuru yule aliyekata bima asipate
hasara na kuyumba pindi anapopata matatizo ya ki afya
Bima ni kinga muhimu ya kumuacha mwenye kukata kuwa na amani ya moyo kwa
kuweza kuwa huru kufanya shughuli zake bila kuhofia mambo yanayoweza kutokea
mbele hata kuharibikiwa ikiwa tayari ameshakata bima ambayo inamlinda pindi
anapopata matatizo ya kiafya.
Bima ya afya pia ni uwekezaji sahihi ambapo
mtumiaji anajiwekea kama dhamana ya kweli yenye manufaa chanya wakati ambao
anakutana na matatizo ya kiafya yasiyoweza kuzuilika . Muhusika wa bima ya afya
anaweza kuyashughulikia masuala yake kwa
haraka bila kuyumba ama kuchukua mkopo.
Bima ya afya ni kama akiba isiyooza ambayo
itatumika katika kipindi ambacho unahitaji msaada wa haraka wa kukuvusha kutoka
sehemu moja kwenda nyingine baada ya mkwamo usiotarajiwa ambao unaweza kupitia
katika maisha yako ya kila siku.
Jamii yetu iko nyuma na haijui umuhimu wa bima ya
afya , Makampuni ya bima yanatakiwa kutumia njia ambazo ni rahisi kuwafikishia
ujumbe wa mara kwa mara wateja wao na kuwafahamisha huduma na mambo mengine
muhimu ya bima.Kuna njia nyingi za kuwafahamisha wateja ama watumiaji taarifa
za bima kwa urahisi usiohitaji kutumia gharama kubwa . Kuwapa taarifa mpya
ambazo zinaweza kuwasaidia katika masuala yote yanayohusu Bima ya afya. zaidi
0 Comments:
Post a Comment