Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali
yanayoweza kuyapata macho.
Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na
pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa
jumla.
Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana
kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha
mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa
kukosa chakula kwa sababu haoni.
Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine
yanasababishwa na nzi, kama vile trakoma, na mengine yanasababishwa
na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua, runinga na hata tarakilishi ambavyo
vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona
karibu na pia kichwa kuuma.
Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa
mishipa ya siliari inayoshika lenzi ya jicho.
Magonjwa yote ya macho yanatibika; inategemea hatua ya ugonjwa huo
wa macho ulipofikia, kama kuona karibu unaweza kupona kwa kutumia lenzi
mbonyeo na kuona mbali unatumia lenzi mbinuko kwenye miwani yako
ambapo humsaidia mgonjwa kuona vizuri na kuweza kutofautisha vitu
mbalimbali na pia ukihisi kama macho yako yanauma unaweza ukala karoti kwa
sababu ina Vitamini A inayoweza kukusaidia ukiwa na ukavu macho.
Magonjwa ya macho yanatibika ukiwahi hospitali kwa matibabu zaidi.
0 Comments:
Post a Comment