Ini Ni Kiungo Muhimu
Sana Ndani Ya Miili Yetu, Hufanya Kazi Zaidi Ya 500 ; Moja Ya Kazi Ni Kuchuja
Na Kuondoa Sumu Kutoka Kwenye Damu.
Kutokana Na Sababu
Mbalimbali Kama Pombe Iliyopita Kiasi, Sumu Kwenye Damu Au Maambukizi; Ini
Hupata Shida Na Kuvimba Na Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri. Hii Hali Huitwa HOMA
YA INI Au HEPATITIS.
Katika Maeneo Yetu,
Bara La Afrika Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini Ndio Sababu Kuu Ya Shida
Kwenye Ini. Virusi Vya Homa Ya Ini Vipo Vya Aina 5 (A,B,C,D,E).
Aina Mbili Za Virusi
(B Na C ) Ndio Sababu Kuu Za Ugonjwa Wa Homa Ya Ini Na Husambaa Kupitia Damu Na
Majimaji Ya Mwili.
Homa Ya Ini Ni Sawa
Janga Linaloua Kimya Kimya Kulingana Na Takwimu Za Vifo Za Dunia Inakadiriwa
Kirusi Cha Homa Ya Ini Aina Ya B Pekee Huua Watu 600,000 Hivi Kila Mwaka.
Kwa Wastani Zaidi Ya
Watu Bilioni Mbili, Yaani, Asilimia 33 Hivi Ya Watu Wote Ulimwenguni,
Wameambukizwa Virusi Vya HBV, Na Wengi Wao Hupona Baada Ya Miezi Michache. Watu
Milioni 350 Hivi Huendelea Kuwa Na Virusi Hivyo Mwilini, Wengi Huishi Bila
Dalili Na Kuendelea Kuambukiza Watu Wengine
NAMNA
GANI UNAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI (B NA C)…….?
Virusi Vya
Homa Ya Ini B Na C Husambaa Kupitia Damu, mbegu za kiume Au Maji Maji Mengine
Ya Mwili.
Virusi Hivi
Vina Uwezo Wa Kusambaa Na Kuambukiza Mtu Mara 100 Zaidi Ya Virusi Vya UKIMWI.
Njia Hizi
Husambaza Virusi Hivi Vya Homa Ya Ini..:
Kutoka Kwa Mama Kwenda Kwa Mtoto
➡️Mama Aliye Na Maambukizi Ya Hepatitis B Kumuambukiza Mtoto
Wakati Wa Kujifungua, Iwapo Hamna Juhudi Za Kitiba Za Kuzuia Maambukizi Kuna
Uwezekano Hadi Asilimia 90 Kwa Mama Kumuambukiza Mtoto.
Kufanya Mapenzi Na Mtu Mwenye Maambukizi Ya Virusi Vya Homa
Ya Ini
Kuchangia Vifaa Vyenye Ncha Kali Kama Sindano Hasa Kwa
Watumia Madawa Ya Kulevya Au Wachora Tattoo, Miswaki
Kuongezewa Damu Ambayo Ina Maambukizi Ya Homa Ya Ini.
Virusi
Vya Homa Ya Ini Vinaweza Ishi Nje Ya Mwili Kwa Muda Mrefu…
Tafiti
Zinaonyesha Virusi Vya Homa Ya Ini Vinaweza Ishi Nje Ya Mwili Hadi Kwa Muda Wa
Siku 7, Bado Vikiwa Na Uwezo Wa Kuambukiza Mtu. Tafiti Zimeonyesha Hata
Iliyokauka Huwa Na Uwezo Wa Kuambukiza Virusi Hivi.
Iwapo Kuna Damu Imemwagika Inatakiwa Isafishwe Na Chlorine
Au Spirit Ili Kuua Virusi
NANI
YUPO KATIKA HATARI ZAIDI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA HOMA YA INI?
* Watoto Wachanga Waliozaliwa Na Mama
Aliye Na Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini
* Watu Wanaofanya Biashara Ya
Ngono
* Wanaume Wanaofanya Mapenzi Na
Wanaume Wenzao
* Watu Wanaojidunga Dawa Za Kulevya
* Mtu Mwenye Mpenzi Ambaye Anaishi Na
Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini
* Wafanyakazi Wa Sekta Ya Afya
* Watu Wa Familia Wenye Ndugu
Anayeishi Na Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini
* Wagonjwa Wa Figo Wanaotumia
Huduma Za Kusafisha Damu (Dialysis)
UGONJWA
WA VIRUSI VYA HOMA YA INI HUJA NA DALILI MBALIMBALI…..
Dalili
Za Muda Mfupi (Acute Hepatitis)
➡️ Dalili Hizi Za Mwanzo Hutokea Ndani Ya Miezi 6 Baada
Kuambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini, Hutokea Kwa Baadhi Ya Watu Hazitokei Kwa
Kila Mtu.
Mgonjwa Mwenye Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini
Hujiskia Kuumwa
* Hupoteza hamu ya kula
* Kichefuchefu na kutapika
* Mwili kuumaMkojo kuwa na rangi iliyokolea kama Coca-Cola
* Kupata manjano kwenye macho, vinganja vya mikono/kucha au
mwili mzima
Kuna Kundi Dogo La Wagonjwa Wa Homa Ya Ini
Hupata Ugonjwa Mkali Wa Ini Na Kusababisha Ini Kushindwa Kabisa Kufanya Kazi
Pia Huweza Kusababisha Kifo. Hii Hatua Huitwa “Fulminant Liver Failure”.
Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini (Chronic
Hepatitis)
Watu Wenye Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini
Mara Nyingi Huwa Hawana Dalili, Kadri Muda Unavyoenda Virusi Husababisha Ini
Kusinyaa (Cirrhosis) Na Kushindwa Kufanya Kazi Vyema.
Pia Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Huchangia Pia
Kupata Saratani Ya Ini.
Kwa
Nini Ni Muhimu Kupima Ili Kujua Kama Una Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini?
….
Watu Wengi Huishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini
Bila Kufahamu. Kwa Kawaida Katika Kipindi Fulani Cha Maisha Mtu 1 Kati Ya Watu
3 Huambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini. Baada Ya Kuambukizwa, Kuna Kundi La Watu
Hubaki Na Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Ambayo Huwa Hayana
Dalili Yoyote Na Kuendelea Kuua Ini Kimyakimya. Dalili Huja Kuonekana Waziwazi
Miaka Mingi Baada Ya Mtu Kuambukizwa. Huonekana Wakati Tayari Ini Limenyauka Au
Lina Kansa.
Hivyo Mtu Aliye Na Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa
Ya Ini Aina B Akianza Matibabu Mapema, Anaweza Kuzuia Ini Lake Lisiharibike
Sana. Pia Kwa Wenye Maambukizi Ya Virusi Aina C Matibabu Ya Dawa Wiki 12
Humaliza Virusi Vyote.
NANI ANAHITAJI KUPIMWA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI?
Watu Kutoka Makundi Yafuatayo Ni Sharti
Kupimwa Kama Wana Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini……
Watu Wanaoishi Kwenye Maeneo Yenye Maambukizi Ya Virusi Vya
Homa Ya Ini Kwa Zaidi Ya Asilimia 2. -Tanzania Ni Moja Ya Nchi Zenye Kiwango
Cha Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Kwa Wastani Wa 5% Hivyo Watanzania
Wote Ni Muhimu Kupima
* Watu Wote
Wanaotumia Dawa Za Kulevya Na Kujidunga
*
Wafanyakazi Katika Sekta Ya Afya
* Watu Wote
Wanaoishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI
* Watu Wote
Ndani Ya Familia Wanaoshi Na Ndugu Aliyeambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini
* Watu Wote
Wanaotumia Dawa Za Kufubaza Kinga Ya Mwili (Immunosuppressive Therapy)
* Watu Wote
Wenye Ugonjwa Wa Figo Wanahitaji Kuanza Dialysis
* Kina Mama
Wajawazito Wote
* Wanaume
Wanaofanya Mapenzi Na Wanaume Wenzao.
UGONJWA
WA HOMA YA INI HUWA NA MATOKEO MABAYA…..
Kwa Wastani Watu 25 Kati Ya 100 Walioambukizwa Virusi Vya
Homa Ya Ini Wakiwa Watoto Na 15 Kati Ya 100 Waliopata Maambukizi Ya Kudumu Ya
Homa Ya Ini Baada Ya Utoto Hufariki Wakiwa Na Umri Mdogo Kwa Ugonjwa Wa Ini
(Ini Kushindwa Kufanya Kazi) Au Saratani Ya Ini.
CHANJO
YA DHIDI YA VIRUSI VYA HOMA YA INI
Watu Kutoka Makundi Yafuatayo Ni Sharti
Kupimwa Kama Wana Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini……
Watu Wanaoishi Kwenye Maeneo Yenye Maambukizi Ya Virusi Vya
Homa Ya Ini Kwa Zaidi Ya Asilimia 2. -Tanzania Ni Moja Ya Nchi Zenye Kiwango
Cha Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Kwa Wastani Wa 5% Hivyo Watanzania
Wote Ni Muhimu Kupima
* Watu Wote
Wanaotumia Dawa Za Kulevya Na Kujidunga
*
Wafanyakazi Katika Sekta Ya Afya
* Watu Wote
Wanaoishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI
* Watu Wote
Ndani Ya Familia Wanaoshi Na Ndugu Aliyeambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini
* Watu Wote
Wanaotumia Dawa Za Kufubaza Kinga Ya Mwili (Immunosuppressive Therapy)
* Watu Wote
Wenye Ugonjwa Wa Figo Wanahitaji Kuanza Dialysis
* Kina Mama
Wajawazito Wote
* Wanaume
Wanaofanya Mapenzi Na Wanaume Wenzao.
0 Comments:
Post a Comment