Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali yanayoweza kuyapata macho. Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa jumla. Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa kukosa chakula kwa sababu haoni. Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine yanasababishwa na nzi, kama vile trakoma, na mengine yanasababishwa na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua, runinga na hata tarakilishi ambavyo vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona karibu na pia kichwa kuuma. Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa mi...
Ini Ni Kiungo Muhimu Sana Ndani Ya Miili Yetu, Hufanya Kazi Zaidi Ya 500 ; Moja Ya Kazi Ni Kuchuja Na Kuondoa Sumu Kutoka Kwenye Damu. Kutokana Na Sababu Mbalimbali Kama Pombe Iliyopita Kiasi, Sumu Kwenye Damu Au Maambukizi; Ini Hupata Shida Na Kuvimba Na Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri. Hii Hali Huitwa HOMA YA INI Au HEPATITIS. Katika Maeneo Yetu, Bara La Afrika Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini Ndio Sababu Kuu Ya Shida Kwenye Ini. Virusi Vya Homa Ya Ini Vipo Vya Aina 5 (A,B,C,D,E). Aina Mbili Za Virusi (B Na C ) Ndio Sababu Kuu Za Ugonjwa Wa Homa Ya Ini Na Husambaa Kupitia Damu Na Majimaji Ya Mwili. Homa Ya Ini Ni Sawa Janga Linaloua Kimya Kimya Kulingana Na Takwimu Za Vifo Za Dunia Inakadiriwa Kirusi Cha Homa Ya Ini Aina Ya B Pekee Huua Watu 600,000 Hivi Kila Mwaka. Kwa Wastani Zaidi Ya Watu Bilioni Mbili, Yaani, Asilimia 33 Hivi Ya Watu Wote Ulimwenguni, Wameambukizwa Virusi Vya HBV, Na Wengi Wao Hupona Baada Ya Miezi Michache. Watu Milioni 350 Hivi Huendelea Kuwa N...