Facebook

Friday, October 27, 2023

HUU NDO UMUHIMU WA KUKATA BIMA KWA JAMII

 


Ikiwa ni miaka 52 sasa toka kuanzishwa shirika la bima hapa nchini, bado watu wengi nchini Tanzania hawana uelewa juu ya masuala ya bima ya afya. Mengi yametajwa kuwa chanzo cha wengi kushindwa kujisajili ama kukata bima ya afya  nchini. Miongoni mwa sababu zinazotajwa sana ni ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu bima , umaskini uliotopea wa kutokujua umuhimu wa bima ya afya katika dunia ya leo.
Ukweli haupingiki kuwa kukata bima ya afya  kunahitaji kuwa na pesa na ni gharama kiasi lakini kwa kuangalia faida zake kwa mahitaji ya mbeleni ni wazi ni jambo mtambuka kulifanya.
Bima ya  afya ni mkataba wenye taswira mbili kwa upande mmoja unaofanana sana na aina nyingine za mikataba kama ilivyo kwa mkataba wa watu wawili kuuziana baiskeli kuingia ubia ili kushirikiana katika kuendesha biashara na kadhalika.

Malengo makuu ya uwepo wa bima ya afya  ni kumnusuru yule aliyekata bima asipate hasara na kuyumba pindi anapopata matatizo  ya ki afya  Bima ni kinga muhimu ya kumuacha mwenye kukata kuwa na amani ya moyo kwa kuweza kuwa huru kufanya shughuli zake bila kuhofia mambo yanayoweza kutokea mbele hata kuharibikiwa ikiwa tayari ameshakata bima ambayo inamlinda pindi anapopata matatizo ya kiafya.

 Bima  ya afya pia ni uwekezaji sahihi ambapo mtumiaji anajiwekea kama dhamana ya kweli yenye manufaa chanya wakati ambao anakutana na matatizo ya kiafya yasiyoweza kuzuilika . Muhusika wa bima ya afya  anaweza kuyashughulikia masuala yake kwa haraka bila kuyumba ama kuchukua mkopo.
Bima ya afya ni kama akiba isiyooza ambayo itatumika katika kipindi ambacho unahitaji msaada wa haraka wa kukuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine baada ya mkwamo usiotarajiwa ambao unaweza kupitia katika maisha yako ya kila siku.
Jamii yetu iko nyuma na haijui umuhimu wa bima ya afya , Makampuni ya bima yanatakiwa kutumia njia ambazo ni rahisi kuwafikishia ujumbe wa mara kwa mara wateja wao na kuwafahamisha huduma na mambo mengine muhimu ya bima.Kuna njia nyingi za kuwafahamisha wateja ama watumiaji taarifa za bima kwa urahisi usiohitaji kutumia gharama kubwa . Kuwapa taarifa mpya ambazo zinaweza kuwasaidia katika masuala yote yanayohusu Bima ya afya. zaidi 

Tuesday, October 24, 2023

YAFAHAMU AINA YA MAGONJWA YA MACHO

 


Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali yanayoweza kuyapata macho.

Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa jumla.

Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa kukosa chakula kwa sababu haoni.

Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine yanasababishwa na nzi, kama vile trakoma, na mengine yanasababishwa na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua, runinga na hata tarakilishi ambavyo vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona karibu na pia kichwa kuuma.

Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa mishipa ya siliari inayoshika lenzi ya jicho.

Magonjwa yote ya macho yanatibika; inategemea hatua ya ugonjwa huo wa macho ulipofikia, kama kuona karibu unaweza kupona kwa kutumia lenzi mbonyeo na kuona mbali unatumia lenzi mbinuko kwenye miwani yako ambapo humsaidia mgonjwa kuona vizuri na kuweza kutofautisha vitu mbalimbali na pia ukihisi kama macho yako yanauma unaweza ukala karoti kwa sababu ina Vitamini A inayoweza kukusaidia ukiwa na ukavu macho.

Magonjwa ya macho yanatibika ukiwahi hospitali kwa matibabu zaidi.