Facebook

Friday, January 5, 2024

gsgjshjhasjak


 
FFSHSYdkmcjkjkcjcljcj jcjz,cj,zcjmjck j

Friday, December 1, 2023

Saturday, November 4, 2023

UGONJWA WA HOMA YA INI NA MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU

 




Ini Ni Kiungo Muhimu Sana Ndani Ya Miili Yetu, Hufanya Kazi Zaidi Ya 500 ; Moja Ya Kazi Ni Kuchuja Na Kuondoa Sumu Kutoka Kwenye Damu.

Kutokana Na Sababu Mbalimbali Kama Pombe Iliyopita Kiasi, Sumu Kwenye Damu Au Maambukizi; Ini Hupata Shida Na Kuvimba Na Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri. Hii Hali Huitwa HOMA YA INI Au HEPATITIS.

Katika Maeneo Yetu, Bara La Afrika Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini Ndio Sababu Kuu Ya Shida Kwenye Ini. Virusi Vya Homa Ya Ini Vipo Vya Aina 5 (A,B,C,D,E).

Aina Mbili Za Virusi (B Na C ) Ndio Sababu Kuu Za Ugonjwa Wa Homa Ya Ini Na Husambaa Kupitia Damu Na Majimaji Ya Mwili.

Homa Ya Ini Ni Sawa Janga Linaloua Kimya Kimya Kulingana Na Takwimu Za Vifo Za Dunia Inakadiriwa Kirusi Cha Homa Ya Ini Aina Ya B Pekee Huua Watu 600,000 Hivi Kila Mwaka.

Kwa Wastani Zaidi Ya Watu Bilioni Mbili, Yaani, Asilimia 33 Hivi Ya Watu Wote Ulimwenguni, Wameambukizwa Virusi Vya HBV, Na Wengi Wao Hupona Baada Ya Miezi Michache. Watu Milioni 350 Hivi Huendelea Kuwa Na Virusi Hivyo Mwilini, Wengi Huishi Bila Dalili Na Kuendelea Kuambukiza Watu Wengine

NAMNA GANI UNAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI (B NA C)…….?

Virusi Vya Homa Ya Ini B Na C Husambaa Kupitia Damu, mbegu za kiume Au Maji Maji Mengine Ya Mwili.

Virusi Hivi Vina Uwezo Wa Kusambaa Na Kuambukiza Mtu Mara 100 Zaidi Ya Virusi Vya UKIMWI.

Njia Hizi Husambaza Virusi Hivi Vya Homa Ya Ini..:

Kutoka Kwa Mama Kwenda Kwa Mtoto
️Mama Aliye Na Maambukizi Ya Hepatitis B Kumuambukiza Mtoto Wakati Wa Kujifungua, Iwapo Hamna Juhudi Za Kitiba Za Kuzuia Maambukizi Kuna Uwezekano Hadi Asilimia 90 Kwa Mama Kumuambukiza Mtoto.

 

Kufanya Mapenzi Na Mtu Mwenye Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini

Kuchangia Vifaa Vyenye Ncha Kali Kama Sindano Hasa Kwa Watumia Madawa Ya Kulevya Au Wachora Tattoo, Miswaki

Kuongezewa Damu Ambayo Ina Maambukizi Ya Homa Ya Ini.

 

Virusi Vya Homa Ya Ini Vinaweza Ishi Nje Ya Mwili Kwa Muda Mrefu…

Tafiti Zinaonyesha Virusi Vya Homa Ya Ini Vinaweza Ishi Nje Ya Mwili Hadi Kwa Muda Wa Siku 7, Bado Vikiwa Na Uwezo Wa Kuambukiza Mtu. Tafiti Zimeonyesha Hata Iliyokauka Huwa Na Uwezo Wa Kuambukiza Virusi Hivi.



Iwapo Kuna Damu Imemwagika Inatakiwa Isafishwe Na Chlorine Au Spirit Ili Kuua Virusi 

NANI YUPO KATIKA HATARI ZAIDI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA HOMA YA INI?  

*  Watoto Wachanga Waliozaliwa Na Mama Aliye Na Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini 

 *  Watu Wanaofanya Biashara Ya Ngono

*   Wanaume Wanaofanya Mapenzi Na Wanaume Wenzao

*   Watu Wanaojidunga Dawa Za Kulevya

*   Mtu Mwenye Mpenzi Ambaye Anaishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini

*   Wafanyakazi Wa Sekta Ya Afya

*   Watu Wa Familia Wenye Ndugu Anayeishi Na Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini

*    Wagonjwa Wa Figo Wanaotumia Huduma Za Kusafisha Damu (Dialysis)

 

UGONJWA WA VIRUSI VYA HOMA YA INI HUJA NA DALILI MBALIMBALI…..

   

Dalili Za Muda Mfupi (Acute Hepatitis)

   

️ Dalili Hizi Za Mwanzo Hutokea Ndani Ya Miezi 6 Baada Kuambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini, Hutokea Kwa Baadhi Ya Watu Hazitokei Kwa Kila Mtu.

Mgonjwa Mwenye Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Hujiskia Kuumwa

* Hupoteza hamu ya kula

* Kichefuchefu na kutapika

* Mwili kuumaMkojo kuwa na rangi iliyokolea kama Coca-Cola

* Kupata manjano kwenye macho, vinganja vya mikono/kucha au mwili      mzima



Kuna Kundi Dogo La Wagonjwa Wa Homa Ya Ini Hupata Ugonjwa Mkali Wa Ini Na Kusababisha Ini Kushindwa Kabisa Kufanya Kazi Pia Huweza Kusababisha Kifo. Hii Hatua Huitwa “Fulminant Liver Failure”.

 

Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini (Chronic Hepatitis)

Watu Wenye Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Mara Nyingi Huwa Hawana Dalili, Kadri Muda Unavyoenda Virusi Husababisha Ini Kusinyaa (Cirrhosis) Na Kushindwa Kufanya Kazi Vyema.



Pia Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Huchangia Pia Kupata Saratani Ya Ini.

 

 

 

Kwa Nini Ni Muhimu Kupima Ili Kujua Kama Una Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini? ….

Watu Wengi Huishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Bila Kufahamu. Kwa Kawaida Katika Kipindi Fulani Cha Maisha Mtu 1 Kati Ya Watu 3 Huambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini. Baada Ya Kuambukizwa, Kuna Kundi La Watu Hubaki Na Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Ambayo Huwa Hayana Dalili Yoyote Na Kuendelea Kuua Ini Kimyakimya. Dalili Huja Kuonekana Waziwazi Miaka Mingi Baada Ya Mtu Kuambukizwa. Huonekana Wakati Tayari Ini Limenyauka Au Lina Kansa.

Hivyo Mtu Aliye Na Maambukizi Ya Kudumu Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Aina B Akianza Matibabu Mapema, Anaweza Kuzuia Ini Lake Lisiharibike Sana. Pia Kwa Wenye Maambukizi Ya Virusi Aina C Matibabu Ya Dawa Wiki 12 Humaliza Virusi Vyote.

 

NANI ANAHITAJI KUPIMWA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI? 

 



Watu Kutoka Makundi Yafuatayo Ni Sharti Kupimwa Kama Wana Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini……  

Watu Wanaoishi Kwenye Maeneo Yenye Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Kwa Zaidi Ya Asilimia 2. -Tanzania Ni Moja Ya Nchi Zenye Kiwango Cha Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Kwa Wastani Wa 5% Hivyo Watanzania Wote Ni Muhimu Kupima

* Watu Wote Wanaotumia Dawa Za Kulevya Na Kujidunga

* Wafanyakazi Katika Sekta Ya Afya

* Watu Wote Wanaoishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI

* Watu Wote Ndani Ya Familia Wanaoshi Na Ndugu Aliyeambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini

* Watu Wote Wanaotumia Dawa Za Kufubaza Kinga Ya Mwili (Immunosuppressive Therapy)

* Watu Wote Wenye Ugonjwa Wa Figo Wanahitaji Kuanza Dialysis

* Kina Mama Wajawazito Wote

* Wanaume Wanaofanya Mapenzi Na Wanaume Wenzao.

 

UGONJWA WA HOMA YA INI HUWA NA MATOKEO MABAYA…..

Kwa Wastani Watu 25 Kati Ya 100 Walioambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini Wakiwa Watoto Na 15 Kati Ya 100 Waliopata Maambukizi Ya Kudumu Ya Homa Ya Ini Baada Ya Utoto Hufariki Wakiwa Na Umri Mdogo Kwa Ugonjwa Wa Ini (Ini Kushindwa Kufanya Kazi) Au Saratani Ya Ini.



CHANJO YA DHIDI YA VIRUSI VYA HOMA YA INI

 





Watu Kutoka Makundi Yafuatayo Ni Sharti Kupimwa Kama Wana Maambukizi Ya Virusi Wa Homa Ya Ini……  

Watu Wanaoishi Kwenye Maeneo Yenye Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Kwa Zaidi Ya Asilimia 2. -Tanzania Ni Moja Ya Nchi Zenye Kiwango Cha Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini Kwa Wastani Wa 5% Hivyo Watanzania Wote Ni Muhimu Kupima

* Watu Wote Wanaotumia Dawa Za Kulevya Na Kujidunga

* Wafanyakazi Katika Sekta Ya Afya

* Watu Wote Wanaoishi Na Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI

* Watu Wote Ndani Ya Familia Wanaoshi Na Ndugu Aliyeambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini

* Watu Wote Wanaotumia Dawa Za Kufubaza Kinga Ya Mwili (Immunosuppressive Therapy)

* Watu Wote Wenye Ugonjwa Wa Figo Wanahitaji Kuanza Dialysis

* Kina Mama Wajawazito Wote

* Wanaume Wanaofanya Mapenzi Na Wanaume Wenzao.

 

UGONJWA WA HOMA YA INI HUWA NA MATOKEO MABAYA…..

Kwa Wastani Watu 25 Kati Ya 100 Walioambukizwa Virusi Vya Homa Ya Ini Wakiwa Watoto Na 15 Kati Ya 100 Waliopata Maambukizi Ya Kudumu Ya Homa Ya Ini Baada Ya Utoto Hufariki Wakiwa Na Umri Mdogo Kwa Ugonjwa Wa Ini (Ini Kushindwa Kufanya Kazi) Au Saratani Ya Ini.

















Friday, October 27, 2023

HUU NDO UMUHIMU WA KUKATA BIMA KWA JAMII

 


Ikiwa ni miaka 52 sasa toka kuanzishwa shirika la bima hapa nchini, bado watu wengi nchini Tanzania hawana uelewa juu ya masuala ya bima ya afya. Mengi yametajwa kuwa chanzo cha wengi kushindwa kujisajili ama kukata bima ya afya  nchini. Miongoni mwa sababu zinazotajwa sana ni ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu bima , umaskini uliotopea wa kutokujua umuhimu wa bima ya afya katika dunia ya leo.
Ukweli haupingiki kuwa kukata bima ya afya  kunahitaji kuwa na pesa na ni gharama kiasi lakini kwa kuangalia faida zake kwa mahitaji ya mbeleni ni wazi ni jambo mtambuka kulifanya.
Bima ya  afya ni mkataba wenye taswira mbili kwa upande mmoja unaofanana sana na aina nyingine za mikataba kama ilivyo kwa mkataba wa watu wawili kuuziana baiskeli kuingia ubia ili kushirikiana katika kuendesha biashara na kadhalika.

Malengo makuu ya uwepo wa bima ya afya  ni kumnusuru yule aliyekata bima asipate hasara na kuyumba pindi anapopata matatizo  ya ki afya  Bima ni kinga muhimu ya kumuacha mwenye kukata kuwa na amani ya moyo kwa kuweza kuwa huru kufanya shughuli zake bila kuhofia mambo yanayoweza kutokea mbele hata kuharibikiwa ikiwa tayari ameshakata bima ambayo inamlinda pindi anapopata matatizo ya kiafya.

 Bima  ya afya pia ni uwekezaji sahihi ambapo mtumiaji anajiwekea kama dhamana ya kweli yenye manufaa chanya wakati ambao anakutana na matatizo ya kiafya yasiyoweza kuzuilika . Muhusika wa bima ya afya  anaweza kuyashughulikia masuala yake kwa haraka bila kuyumba ama kuchukua mkopo.
Bima ya afya ni kama akiba isiyooza ambayo itatumika katika kipindi ambacho unahitaji msaada wa haraka wa kukuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine baada ya mkwamo usiotarajiwa ambao unaweza kupitia katika maisha yako ya kila siku.
Jamii yetu iko nyuma na haijui umuhimu wa bima ya afya , Makampuni ya bima yanatakiwa kutumia njia ambazo ni rahisi kuwafikishia ujumbe wa mara kwa mara wateja wao na kuwafahamisha huduma na mambo mengine muhimu ya bima.Kuna njia nyingi za kuwafahamisha wateja ama watumiaji taarifa za bima kwa urahisi usiohitaji kutumia gharama kubwa . Kuwapa taarifa mpya ambazo zinaweza kuwasaidia katika masuala yote yanayohusu Bima ya afya. zaidi 

Tuesday, October 24, 2023

YAFAHAMU AINA YA MAGONJWA YA MACHO

 


Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali yanayoweza kuyapata macho.

Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa jumla.

Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa kukosa chakula kwa sababu haoni.

Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine yanasababishwa na nzi, kama vile trakoma, na mengine yanasababishwa na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua, runinga na hata tarakilishi ambavyo vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona karibu na pia kichwa kuuma.

Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa mishipa ya siliari inayoshika lenzi ya jicho.

Magonjwa yote ya macho yanatibika; inategemea hatua ya ugonjwa huo wa macho ulipofikia, kama kuona karibu unaweza kupona kwa kutumia lenzi mbonyeo na kuona mbali unatumia lenzi mbinuko kwenye miwani yako ambapo humsaidia mgonjwa kuona vizuri na kuweza kutofautisha vitu mbalimbali na pia ukihisi kama macho yako yanauma unaweza ukala karoti kwa sababu ina Vitamini A inayoweza kukusaidia ukiwa na ukavu macho.

Magonjwa ya macho yanatibika ukiwahi hospitali kwa matibabu zaidi.